Ushirikiano katika matukio makubwa. Kwa mfano, katika siku zijazo tutakuwa na tukio kubwa la kusherehekea Maulidi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w). Sasa umefika wakati wa kuonyesha mshikamano wetu kwa ulimwengu mzima… Hivyo ushirikiano huu uendelee mpaka katika maandalizi ya sherehe ya Maulidi ya Mtume (s.a.w.w) ili kuimarisha umoja wetu.
Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) -ABNA- Katika kikao cha leo na Mufti wa Kishafi wa Taifa la Burundi, tulijadili mambo kadhaa muhimu:
1. Kuimarisha Umoja kati ya Madhehebu ya Shia na Shafi‘i kwa ajili ya kukabiliana na nguvu potovu za Usalafi na Uwahabi ambazo kwa kasi kubwa zinajitahidi kuleta mgawanyiko kati ya Waislamu. Kwa sasa makundi kadhaa ya Kiwahabi yanamshinikiza Mufti wa Kishafi akubali kwamba Mashia ni makafiri ili taifa lote lielewe hivyo. Lakini Mufti amekataa vikali jambo hilo na kamwe hayuko tayari kukubaliana nalo.
2. Ushirikiano wa kimkakati kati ya Shia na Shafi‘i ili kuonyesha mbele ya serikali kwamba sisi Mashafi na Mashia ni kitu kimoja na ni taasisi huru zinazoshirikiana, na tunapaswa kushirikiana kuvunja nguvu ya Kiwahabi.
3. Ushirikiano katika matukio makubwa. Kwa mfano, katika siku zijazo tutakuwa na tukio kubwa la kusherehekea Maulidi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w). Sasa umefika wakati wa kuonyesha mshikamano wetu kwa ulimwengu mzima… Hivyo ushirikiano huu uendelee mpaka katika maandalizi ya sherehe ya Maulidi ya Mtume (s.a.w.w) ili kuimarisha umoja wetu.
Tunawashukuru sana Jumuiya ya Khoja na Jamiat al-Mustafa al-‘Alimiyyah kwa kuandaa kikao hiki cha kutafakari kuhusu mustakabali wa Uislamu.
Your Comment